Obama akosoa ushughulikiaji wa janga la virusi vya corona
17 Mei 2020Obama alizungumza katika kile kinachojulikana kama "Show Me Your Walk" toleo la HBCU," tukio la masaa mawili kwa wanafunzi wanaohitimu kutoka vyuo ambavyo kwa kihistoria ni vya watu wenye asili ya Afrika na vyuo vikuu lililotangazwa katika You Tube, Facebook na Twitter. Matamshi yake yalikuwa bila kutarajiwa ya kisiasa, kutokana na eneo lenyewe, na kugusia kuhusu matukio ya hivi sasa kupindukia virusi na athari zake za kijamii na kiuchumi.
"zaidi ya kila kitu, janga hili hatimaye limetoboa tena pazia kwa ukamilifu wake kuhusu wazo kwamba watu wengi wanaohusika madarakani wanajua kile wanachokifanya," Obama alisema. "Wengi wao hata wanaonekani kujidai kuwa wanawajibika."
Baadaye hiyo jana, wakati wa hotuba ya pili iliyotangazwa katika televisheni, Obama alishutumu "kile kinachofahamika kama watu wazima, ikiwa ni pamoja na baadhi wenye vyeo vya juu na kazi muhimu" ambao wanafanya "kile kinacholeta hisia nzuri, kile kinachoridhisha, kile rahisi."
Obama akosoa
"Ndio sababu mambo yanakwenda ndivyo sivyo," amesema.
Obama hakumtaja rais Donald Trump ama afisa mwingine yeyote wa serikali kuu ama wa kitaifa katika hotuba zake hizo zote. Lakini mapema mwezi huu , alimkosoa vikali Trump katika jinsi anavyolishughulikia suala la janga la virusi vya corona kuwa ni "maafa makubwa yenye mkanganyiko" katika mazungumzo ya simu na wajumbe 3000 wa utawala wake iliyopatikana na Yahoo News.
Matamshi hayo ya kuanza shule ni ishara ya hivi karibuni kabisa kuwa Obama ana nia ya kuchukua jukumu kubwa zaidi katika uchaguzi unaokuja. Alikuwa kimya sana katika miaka tangu alipoondoka madarakani , hata wakati Trump amekuwa akimshambulia. Obama amewaambia waungaji wake mkono kwa njia ya simu kwamba atakuwa "akitumia muda mwingi iwezekanavyo na kufanya kampeni kwa nguvu kwa kadiri ninavyoweza" kwa ajili ya Joe Biden, ambaye alikuwa makamu wake wa rais.