1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama Afrika: Vita dhidi ya ugaidi

24 Julai 2015

Katika ziara ya rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya na Ethiopia, suala la kupambana na ugaidi litakuwa mstari wa mbele kwenye agenda. Marekani pia inatarajia kunufaika na uchumi wa bara la Africa.

https://p.dw.com/p/1G47H
Kenia Nairobi Bus vor Obama Besuch
Picha: Getty Images/AFP/S. Maina

Je hizi ni ishara za "egemeo kwa bara la Afrika?" Mwanzoni mwa wiki, rais Barack Obama alimpokea mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari katika ikulu ya Marekani. Siku chache baade atakuwa ni rais wa kwanza wa Marekani kuzitembelea Kenya na Ethiopia.

Katika mahojiano na DW Richard Downie, mtaalam wa masuala ya Afrika katika kituo cha mikakati na mafunzo ya kimataifa mjini Washington, anakataa kukubali kwamba uhusiano huu mpya ni ushahidi unaothibitisha Marekani sasa inavutiwa na bara la Afrika. Uhusiano ambao utakuwa zaidi ya kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM)

Thamani ya kimkakati kwa Marekani kuwa na mahusiano na vigogo wa Afrika kama Nigeria na Kenya ni dhahir. Pamoja na masilahi ya kiuchumi katika taifa linaloendela kuimarika, Marekani pia inatafuta washirika katika vita vyake dhidi ya ugaidi. Huku tishio la ugaidi likiwa linazidi kutoka upande wa mashariki ya kati, kuna wasiwasi mkubwa vipi bara la Afrika litachangia katika suala hili.

Vita dhidi ya ugaidi

Deutschland G7 Gipfel Elmau Barack Obama und Muhammadu Buhari
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na rais wa Nigeria Muhammadu BuhariPicha: picture-alliance/AP Photo/C. Kaster

Mfano mmoja ni namna sasa kundi la Boko Haram lilivofungamana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS. Na hili ni tishio kubwa kwa usalama wa Nigeria na rais Buhari ambae ameingia madarakani mwezi wa Mei. Downie amesema Kenya ni mshirika wa kibiashara muhimu sana wa Marekani, na pia inabeba jukumu kubwa katika usalama wa kikanda na katika kujadili amani katika baadhi ya migogoro ndani ya kanda hiyo. Wakati huohuo inakabiliana na hali tete ya uslama, ikiwa inapambana na tishio la ugaidi wa kundi la al-Shabab.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema ni wakati mbaya kwa Obama kuitembele Ethiopia. Kwani ni kipindi kifupi tu baada ya uchaguizi wa mwezi Mei ambao chama tawala kilitangazwa kushinda viti vyote ndani ya bunge la nchi hio. Huku upinzani ukilalamika juu ya unyanyasaji. Downie anasema Obama hatoweza kufanikisha mengi katika ziara yake nchini Ethiopia. Obama pia atajaribu kukutana na asasi za kiraia lakini hamna hakika kama hilo litawezekana kwani asasi nyingi za kiraia nchini humo zimezimwa mdomo.

Ushindani na China

Cartoon von Said Michael

Hata hivyo Peter Pham wa Baraza Atlantic la mjini Washington, amesema Obama pia atazungumzia juu ya masuala ya kiuchumi. Afrika ni bara moja linalokuwa haraka kiuchumi. Na Marekani akifika Afrika atamkuta Mchina tayari ameshafika huko.

Yun Sun wa taasisi ya Brookings anasema, Marekani haina mkakatani makini wa kushindana na China. Kuimarisha demokrasia na maadili haitoshi. Inawezekana kuwa viongozi wanaofwata demokrasia wa nchi za Afrika wanauhusiano mzuri na nchi za magharibi, lakini pia China inapopendekeza kuwekeza na kuimarisha miundombinu ndani ya nchi zao, viongozi hawa huwa hawakatai uhusiano na China.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/Gero Schliess/dw

Mhariri: Iddi Ssessanga