1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama aelekea katika ziara Vietnam na Japan

22 Mei 2016

Rais wa Marekani Barack Obama ameondoka jana Jumamosi (21.05.2016)kwenda katika ziara nchini Vietnam na Japan ambayo itajumuisha ziara ya kwanza mjini Hiroshima kwa rais wa Maarekani aliyeko madarakani.

https://p.dw.com/p/1IsSY
USA, Nguyen Phu Trong und Barack Obama
Rais Obama (kulia)akisalimiana na kiongozi wa chama cha kikomunist cha Vietnam Nguyen Phu Trong(kushoto)Picha: Reuters/J. Ernst

Obama amesafiri kwa ndege rasmi ya rais ya Air Force One katika mkondo wa kwanza wa ziara hiyo, ambayo itamalizika kwa kusimama kwa muda kutia mafuta katika kituo cha kijeshi cha Elmendrf katika eneo la Anchorage , jimboni Alaska.

Ziara ya kumi ya rais Obama katika bara la Asia ina lengo la kufunga kurasa mbaya katika vita viwili vya karne ya 20 katika eneo hilo ambalo analiona kuwa muhimu katika hali ya baadaye ya Marekani.

Vietnam Nguyen Phu Trong beim Parteitag in Hanoi
Kiongozi wa chama cha kikomunist nchini Vietnam Nguyen Phu TrongPicha: Reuters/Kham

Ziara hiyo itaanzia Hanoi, ambako Obama atasisitiza kuimarisha uhusiano na nchi hiyo inayojitokeza kwa kasi na kwa nguvu kiuchumi, lakini ni nchi ambayo , kwa Wamarekani wengi , inabakia kwa maneno kuwa nchi ya mauaji na upumbavu.

Suala kuu la mazungumzo litakuwa kuondoa marufuku ya silaha iliyowekwa na Marekani, alama iliyobakia katika vita ambavyo vilimalizika mwaka 1975. Atakutana na rais, waziri mkuu, kiongozi wa bunge la taifa na kiongozi mkuu wa nchi hiyo Nguyen Phu Trong, katibu mkuu wa chama cha kikomunist.

Mivutano ya kugombea maeneo ya habarini

Trong na Obama walikutana Julai mwaka jana, wakati kiongozi huyo wa Vietnam alipopewa fursa adimu ya kukutana na rais wa Marekani katika ofisi kuu ya rais ya Oval mjini Washington. Mivutano mikali kuhusiana na masuala ya maeneo ya baharini kati ya Vietnam na jirani yake mkubwa China huenda pia ikajadiliwa kwa kina.

USA Presskonferenz Obama zur US Wirtschaft
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: Getty Images/AFP/S. Loeb

Wanaotaka vikwazo vya silaha viondolewe wanadai kwamba ni muhimu kuisaidia Vietnam kuimarisha ulinzi wake wa pwani na kuimarisha jeshi lake dhidi ya China.

Nchini Japan , Obama atahudhuria mkutano wa kundi la mataifa ya G7 na kuweka historia kwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kutembelea Hiroshima, ambako mwaka 1945 rais wa wakati huo wa Marekani Harry Truman aliamuru kushambulia kwa bomu la kwanza la kinyuklia duniani.

Ziara hiyo mjini Hiroshima imezusha hata hivyo mjadala juu ya iwapo uamuzi wa Truman ulikuwa wa haki.

Japan Hiroshima Früher und Heute Bildergalerie Bild 7
Mji wa Hiroshima nchini Japan uliposhambuliwa kwa bomu la kinyuklia 1945Picha: Reuters/Masami Oki/Hiroshima Peace Memorial Museum

Wamarekani wengi wanaamini kwamba wakati bomu hilo liliuwa kiasi ya Wajapani 140,000, kuishambulia Hiroshima kwa bomu na kisha Nagasaki kumeepusha uvamizi mkubwa zaidi wa ardhini wa japan.

Wahanga wa mashambulizi hayo ya bomu wametoa wito wa kuombwa msamaha , ambapo Ikulu ya marekani inasema haiko tayari kutoa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani