1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyota wa riadha Kenya Kipchoge akabiliwa na madai ya rushwa

15 Oktoba 2018

Kipchoge Keino ambaye ni bingwa mara 2 wa Olimpiki anatuhumiwa kuhusika na utumiaji mbaya wa fedha za wanariadha wa Kenya.

https://p.dw.com/p/36YN8
Kenia Läufer Kipchoge Keino
Picha: AP

Nyota wa zamani wa riadha nchini Kenya, Kipchoge Keino, ameamriwa kuripoti polisi Jumatatu ya leo, akiwa ni miongoni mwa  watuhumiwa katika uchunguzi unaohusiana na rushwa, ili kufunguliwa mashtaka ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya zaidi ya dola 545,000.

Keino, bingwa mara mbili wa Olimpiki na mwanachama wa heshima wa kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, anatuhumiwa amehusika na utumiaji mbaya wa fedha zilizokusudiwa wanariadha wa Kenya wakati wa michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro - Brazil 2016, alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya.

Fedha hizo ni sehemu ya dola milioni 5 alizopewa Keino na serikali ya Kenya. Kuigharimia timu ya Krenya mjini Rio. Lakini waendesha mashitaka wanasema Keino alikuwa ni kiongozi wa kamati ya Olimpiki iliyojaa rushwa.

Mwanariadha huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 78, alikuwa mmoja wa maafisa 7 wa zamani wa Olimpiki na serikali waliotajwa kuwa watuhumiwa katika uchaguzi juu ya kadhia hiyo.

Miongoni mwa vigogo wanaotuhumiwa ni pamoja na waziri wa zamani wa michezo wa Kenya, Hassan Wario, na maafisa watatu wa wizara waliofanya kazi chini yake.