Wafanyakazi wa umma nchini Tanzania wamevuta pumzi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa taifa hilo kutangaza kurejesha nyongeza ya mishahara ya kila mwaka kwa wafanyakazi hao ikiwa ni miaka saba tangu kuondolewa kwa mfumo huo na Rais wa Awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli mwaka 2016. Sudi Mnette amezungumza na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania-TUCTA, Kheri Mkunda.