1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyimbo za ushabiki wakati wa michuano

10 Juni 2016

Mashabiki wa kandanda wanapenda kuimba, bila kujali matokeo ya uwanjani – na lakini pia baadhi ya wachezaji pia hufanya hivyo. Wakati Euro 2016 imeanza, hizi ni baadhi ya nyimbo zinazopendwa toka zamani.

https://p.dw.com/p/1J4XK
UEFA Champions League Atletico Madrid vs. Bayern München Fans
Picha: Reuters/P. Hanna

Wakati dimba la Euro 2016 likitifua vumbi Ufaransa, hebu nikufahamishe Nyimbo za mashabiki wa Uingereza hasa ndizo maarufu sana, hata ingawa timu yao ya taifa England mara nyingi hurejea nyumbani mikono mitupu kutoka mashindano ya kimataifa. Lakini Uingereza inafahamika kama chimbuko la kandanda lenyewe, na hilo pia ni kweli kwa nyimbo za ushabiki.

Nyimbo maarufu kama "Yellow Submarine" ya The Beatles, "Que Sera Sera" ya Doris Day, au "Go West" ya the Pet Shop Boys aghalabu hutumiwa lakini kwa kuwekwa maneno mapya ya kutungwa kwa kutegemea matokeo ya uwanjani. Hata Ujerumani, nyimbo hizi ni sehemu ya utamaduni wa mkusanyiko.

Kila klabu ya kandanda ina wimbo wake maalum kama kitambulisho. Kwa mfano You'll Never Walk Alone, unaotumiwa na Liverpool, lakini pia na vilabu vya Ujerumani, Ulaya na kwingineko, ikiwemo Borussia Dortmund.

Pia kuna nyimbo kama vile The Three Lions, au Football is coming home unaotumiwa na timu ya kandanda ya England. Lakini wimbo ambao huenda ni maarufu sana ni wa Seven Nation Army, ambao tangu Euro 2008 umekuwa ukirindima ndani ya viwanja vya kandanda hasa kila mara bao linapofungwa.

Lakini kando na mashabiki kuimba nyimbo hizo, pia kuna wachezaji wanaojaribu kuimba, mfano mzuri ni bendi ya Sportfreunde Stiller iliyomtumia nyota Roque Santa Cruz, aliyeichezea Bayern munich kwa miaka nane, na wakaimba wimbo “Ich Roque” mwaka wa 2004. Nyota wa Ujerumani na Arsenal Mesut Özil alishirikiana na Jan Delay kurap wimbo wa “Large” mwaka wa 2010. Nyota wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo, ambaye ameimba wimbo wa Mi Amor, lakini ni wimbo wa mahaba na wala hauhusiani na kandanda. Huenda CR7 ana mipango ya kuwa msanii wa muzii katika maisha yake ya baada ya kutundika njumu

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef