Nusu fainali ya kombe la dunia la wanawake
13 Julai 2011Ni dakika 90 pekee zinazo zitofautisha timu za Ufaransa na Marekani uwanjani Monchengladbach hii leo, kila moja ikiwania nafasi kwenye fainali za mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia.
Ni safari ndefu ziliopitia kufuzu kuingia kiwango hichi cha leo cha nusu fainali kila mmoja ikionesha ushindani mkubwa katika robo fainali zilizomalizika na hatimaye kuchukuwa ushindi kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya Uingereza na Brazil Mtawalia. Baada ya kukivuka kizingiti hicho timu ya Ufaransa na Marekani zina mtihani mwingine hii leo kila mmoja ikiwa na mtindo wake binafsi kulivuka daraja la leo.
Kwa kufanikiwa kuvuka kiwango cha robo fainali, timu ya Marekani imeiendeleza rekodi yake nzuri ya kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano yote ya Kombe la dunia ya shirikisho la kandanda ulimwenguni FIFA.
Ama kwa upande wa mechi ya pili jioni ya leo, Japan inayopambana na Sweden inahesabu miongoni mwa mashabiki wake, wafanyakazi wanaoendelea na jitihada za kurudisha utulivu katika nchi ya Japan iliyokumbwa na mzozo mbaya zaidi duniani katika miaka 25 wa nyuklia .
Mchezaji nyota wa timu ya Japan aliyechangia ushindi wa timu hiyo dhidi ya Ujerumani,Karina Maruyama, amekuwa shujaa wa kitaifa kufuatia bao lake la dakika 108 lililo iondoa timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya mwaka huu.
Kocha wa timu hiyo Norio Sasaki anasema kumbukumbu ya maafa ya tetemeko la ardhi na tsunami nchini mwao linawapa motisha wachezaji wake kufuatia kuwadia mechi ya leo dhidi ya Sweden.
Hii ni mara ya kwanza katika historia Japan imeanguka katika timu nne za mwisho katika mashidano haya.
Ushindi wa timu hiyo ya soka umetawala kurasa za spoti nchini Japan ambazo kwa kawaida hujaa taarifa kuhusu michezo maarufu nchini humo, Sumo na Baseball, na ushindi huo dhidi ya Ujerumani, kapteni Homare Sawa, anasema umeishinikiza timu hiyo kutaka kusogea mbele zaidi.
Kwa upande wake Sweden inaelekea kwenye mashindano ya leo ikiamini kuwa itakabiliana na ushindani mkali na kuwa Japan sio timu ya kudharauliwa.
Mwandishi:Maryam Dodo Abdalla/FIFA.com/Rtre/Afpe/DW -TV.
Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed