1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Norway kuwapokea wahamiaji 600 waliopelekwa Rwanda

9 Januari 2020

Norway mwaka  huu  itawachukua  watu 600 waliopelekwa nchini  Rwanda  kutoka  katika  vituo  vya  kuwashikilia nchini Libya , nchi  hiyo  imesema  Jumatano.

https://p.dw.com/p/3Vx6O
Flüchtlingslager Gashora in Ruanda
Picha: DW/A. Ngarambe

Norway mwaka  huu  itawachukua  watu 600 waliopelekwa nchini  Rwanda  kutoka  katika  vituo  vya  kuwashikilia nchini Libya , nchi  hiyo  imesema  Jumatano wakati ikitafuta kukatisha  tamaa juhudi  za  kuwasafirisha  watu  kwa  njia haramu  kupitia  bahari  ya  Mediterania.

Rwanda, ambako  zaidi  ya  watu  milioni 2 walikimbia makaazi  yao  kutokana  na  mauaji  ya  kimbari  mwaka 1994, ilitia  saini  makubaliano   na  Umoja  wa  Mataifa mwezi  Septemba  yenye lengo la  kusaidia  kuwapa makaazi  watu  walioshikiliwa  nchini  Libya  wakati wakijaribu  kusafiri kwenda  Ulaya.

Wahamiaji  waliopelekwa  nchini  Rwanda  wamepewa hadhi  ya  waomba hifadhi  katika  nchi  hiyo  wakati shirika la  Umoja  wa  Mataifa  la  kuwahudumia  wakimbizi UNHCR  likiamua  iwapo  ni  wakimbizi. Katika  taarifa  kwa shirika  la  habari  la  Reuters, waziri  wa  sheria  wa Norway  Joeran Kallmyr  amesema  idadi  ya  watu watakaochukuliwa  mwaka  2020  ni 600, lakini  aliongeza kuwa  hiyo  haitaelekeza  katika  ongezeko  ya  idadi  jumla ya  wakimbizi  ambao serikali  iliyopita  ilidhamiria.