1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOORDWIJK:Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO waendelea

24 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7D2

Mashambulio yanayoendelea nchini Afghanistan ndilo swala linalopewa kipaumbele katika ajenda ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa nchi 26 wanachama wa jumuiya ya kujihami ya magharibi NATO unaoendelea nchini Uholanzi.

Marekani na Uingereza zinawataka washirika wake wa nchi za Ulaya kuzidisha idadi ya wanajeshi wao na vifaa vya vita kwa ajili ya kupambana na waasi wa kundi la Taliban nchini Afghanistan.

Wadadisi wanasema kuwa hatua ya Marekani na Uingerzea huenda ikagonga mwamba.

Mawaziri hao wa NATO pia wanajadili mpango wa Marekani wa kutaka kuwekeza mitambo ya kinga dhidi ya makombora katika nchi za Ulaya ya Mashariki za Poland na Jamuhuri ya Czech.

Marekani inatetea mpango wake huo kwa kusema kuwa unalenga kuzuia mashambulio kutoka Iran lakini Moscow inapinga vikali pendekezo hilo.