Njia ya pekee ni juu: Viwanja vya ndege duniani kwa picha
Kadri watu wanavyozidi kusafiri kwa ndege, viwanja vya ndege navyo lazima vipanuliwe. Katika miaka miwili ijayo China itakuwa na uwanja mkubwa wa ndege duniani ila wengine nao wana mikakati hiyo.
Unatarajiwa kuwa uwanja mkubwa zaidi duniani
Beijing-Daxing unakadiriwa kuhimili wasafiri milioni 100 kwa mwaka itakapokuwa tayari. Baada ya kufunguliwa kwake kunakotarajiwa Oktoba mwaka 2019 ni wasafiri milioni 45 watapitia uwanja huo wa ndege kwa mwaka. Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola bilioni 10.
Uwanja wa ndege uliojengwa sehemu ya juu zaidi duniani
Ukiwa katika sehemu iliyo na urefu wa mita 4,411 juu ya usawa wa bahari, uwanja wa Daocheng Yading umeichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na uwanja wa ndege wa Bangda katika eneo la Tibet, uliokuwa sehemu ya juu zaidi. Eneo hilo ni mlango wa kuingia Tibet, na China inatafuta njia za kukuza utalii kama njia moja ya kupunguza malalamiko kutoka kwa Watibet wenyewe.
Pale Mashehe wanaposafiri
... na watalii wengi na wafanyabiashara. Huku ukiwa na uwezo wa kuwahudumia wasafiri milioni 83, uwanja huo wa nyumbani wa ndege za Emirates - Uwanja wa Kimataifa wa Dubai - ndio uwanja wa tatu mkubwa duniani. Ndio njia kuu ya kuingia Asia Mashariki, India na Australia.
Atlanta inavunja rekodi mpya
Karibu wasafiri 104 walisafirishwa kutoka hapa mwaka 2016. Mwaka mmoja awali, Atlnta ulikuwa uwanja uliohudumia zaidi ya wasafiri milioni 100 kwa mwaka - hiyo ni rekodi ya dunia.
Uwanja nambari moja Ulaya
Uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London - ukiwa uliwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 75 mwaka 2016 - ndio uwanja mkubwa zaidi Ulaya. Maeneo mapya ya kuwapokea wasafiri yanajengwa na yale ya kitambo kuvunjwa. iwapo eneo la sita la kuwapokea wasafiri litaongezwa, basi huenda idadi ya wale wanaosafiri kupitia uwanja huo wa ndege ikafikia wasafiri milioni 115 kwa mwaka.
Uwanja nambari mbili Ulaya
Karibu watu milioni 66 walisafiri kwa kupitia uwanja huu mwaka 2016. Jambo hili linaufanya uwanja wa Charles de Gaulle kuwa wa pili kwa ukubwa Ulaya na wa tisa duniani.
Uwanja mkubwa zaidi Ujerumani
... uko mjini Frankfurt. Karibu watu milioni 60 wanasafiri kupitia uwanja wa Rhein-Main kila mwaka. Kidunia ni uwanja unaoorodheshwa wa 13 kwa ukubwa. Mipango ya kuuongeza inafanywa ili kiwango cha wasafiri wanaotumia uwanja huo kiongezwe hadi kifikie milioni 73.
Treni inayoshikiliwa na sumaku inahitaji umakini
Shanghai ndiyo uwanja wa ndege watatu kwa ukubwa China, huku ukiwa unawahudumia wasafiri milioni 66 kwa mwaka. Uwanja mkuu wa sasa (Beijing Capital Airport, unaowahudumia wasafiri milioni 94 kwa mwaka, ndio wa pili kwa ukubwa duniani). Uwanja wa Shanghai Pudong ni maarufu kwa kuwa una treni inayoshikiliwa na sumaku, na treni hiyo inawapeleka wasafiri katika mji wa kisasa wa Pudong.
BER Berlin: pie iliyo mbinguni
Ni mdogo sana ukilinganishwa na viwanja vya ndege vilivyotajwa awali, kwa kuwa utakaomalizwa wasafiri milioni 22 watakuwa wanapitia uwanja wa Berlin kwa mwaka, lakini majengo ya kuupanua uwanja huo tayari yameanza kupangiwa mwaka 2035 hatua itakayoongeza uwezo wake na uhudumie wasafiri milioni 58 kwa mwaka. Ni matumaini kwamba mipango ya baadae ya ujenzi itakwenda vyema zaidi kushinda ya awali.
Uwanja wa ndege unaowafaa wachache zaidi duniani.
Uwanja wa ndege wa Mtakatifu Helena katika kisiwa cha Mtakatifu Helena uliidhinishwa mwaka 2016 na ndege ya kwanza ya kimataifa kuondoka uwanja huo ilipaa tarehe 14 Oktoba mwaka 2017. Hauwezi kuwa mmoja wa viwanja vya ndege vikubwa zaidi duniani. Baadhi ya vyombo vya habari vya Uingereza vimeuelezea kama "uwanja usio na maana zaidi duniani."