Chama cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani cha Christian Democratic Union - CDU kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwisho wa majimbo kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza katika miaka 16 bila kumhusisha kansela huyo. Sudi Mnette amezungumza na Abdul Mtullya, ambaye ni mjuzi wa sisa za Ujerumani na kwanza alimuuliza ushindi huo unatoa taswira gani kwa CDU?