Maoni mbele ya Meza ya duara, wiki hii yanaumilika mgogoro mkubwa mkoani Tigray dhidi ya vikosi vya shirikisho la Ethiopia. Jumuiya ya kimataifa imeitolea wito taifa hilo kuumaliza mzozo huo kwa njia za kidiplomasia, mwito ambao umepuuzwa na waziri mkuu Abiy Ahmed. Janga la kibinadamu linatajwa kunukia, je nini kipo nyuma ya mgogoro huo? Ungana naye Saumu Mwasimba na wageni washiriki.