Nilikuwa mfungwa wa kisiasa - Assange
1 Oktoba 2024Akizungumza mbele ya Kamati ya Kutetea Haki za Binaadamu ya Baraza la Umoja wa Ulaya, Julian Assange alisisitiza kuwa hakuwa na hatia yoyote ya kumfanya ashikiliwe kizuizini kwa miaka kadhaa.
Assange alizungumza kwa mara ya kwanza hadharani tangu alipoachiwa huru kutoka jela baada ya kufikia makubaliano na Marekani.
Soma zaidi: Assange arejea nchini mwake baada ya kuachiliwa huru
Mwasisi huyo wa mtandao wa WikiLeaks aliiambia kamati hiyo mjini Strasbourg kwamba aliachiwa huru sio kwa sababu mfumo wa sheria unafanya kazi bali ni kw asababu alikubali kukiri kufanya kosa la kuwa mwandishi habari, baada ya kukaa jela kwa miaka kadhaa.
Assange aliachiliwa huru baada ya kukaa jela miaka mitano nchini Uingereza, alipokubali kukiri kuzipata na kuchapisha siri za jeshi la Marekani.