Nigeria kuanza kutowa chanjo ya Mpox kuanzia Oktoba 8
1 Septemba 2024Matangazo
Nigeria ilipokea dozi shehena ya kwanza ya dozi 10,000 ya chanjo hiyo kutoka shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani siku ya Jumanne wiki hii.
Msemaji wa shirika la maendeleo ya afya ya msingi nchini Nigeria Remi Adeleke amesema chanjo zilizowasili lazima zifanyiwe utafuti wa kimaabara nchini humo kwa kipindi cha wiki tatu na baadae zitaanzakusambazwa katika majimbo matano ambako watu 4,750 watachanjwa,kila mmoja atapata dozi mbili katika muda wa siku 28.
Adeleke amesema wanalenga kutoa chanjo hizo kwa wale walioko kwenye muingiliano wa karibu na walioambukizwa virusi vya Mpox, wafanyakazi wa afya pamoja na watu wenye kinga dhaifu kiafya.