Nigeria yatandikwa mabao 2-0 na Croatia
17 Juni 2018Matangazo
Kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio ameahidi timu yake itawabana mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani, wakati timu hizo mbili zikikutana kwenye mchezo wao wa kwanza leo Jumapili.
Mexico wamewahi kuishinda Ujerumani mara moja katika majaribio 11. Walishinda 2-0 katika mechi ya kirafiki mwaka 1985, lakini Osorio anaamini wachezaji wake wanapaswa kupuuza rekodi mbaya ya timu yake dhidi ya mabingwa wa dunia mara nne.
Katika mechi za jana Jumamosi Ufaransa iliifunga Australia mabao 2-1, Argentina ilitoka sare ya bao 1-1 na Iceland, Denmark iliifunga Peru bao 1-0 na wawakilishi wengine wa Afrika Nigeria walitandikwa mabao 2-0 na Croatia.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni kati ya Costa Rica na Serbia na Brazil wanavaana na Uswisi.