1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yapitisha sheria kuzuwia utakatishaji fedha

Sekione Kitojo
31 Mei 2017

Wabunge nchini Nigeria wamepitisha muswad wa sheria wenye lengo la kuzuwia utakatishaji fedha kwa kuzitaka nchi za kigeni, ambako wahalifu wanaohusika na fedha wanajificha, kushirikiana kwa kuwashitaki.

https://p.dw.com/p/2dvN1
Muhammadu Buhari Nigeria
Picha: picture alliance/AP Photo/S.Alamba

Kwa mujibu wa muswada  huo, Nigeria huenda ikaitaka nchi yoyote ambako mtu anayehusika na utakatishaji wa fedha na yule  anajificha kusaidia, kumshitaki mhalifu huyo, ama imshitaki mtu huyo  binafsi. 

Katika hatua ya pili, Nigeria itaipatia nchi hiyo ushahidi wa kuweza kumhukumu. Maendeleo katika nchi hiyo mwanachama  wa Shirika la Mataifa Yanayosafirisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) na yenye uchumi mkubwa barani Afrika, yamekumbwa  na rushwa iliyokithiri. 

Wengi wa  watu wanaishi chini ya dola moja  kwa  siku licha ya utajiri mkubwa wa nishati nchini humo, sehemu kubwa ikiwa imeporwa na watu wachach  matajiri.