1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yajiweka vizuri kufuzu kwenda Urusi

Sekione Kitojo
4 Septemba 2017

Barani Afrika timu zinajiwinda kuwania kufuzu kucheza dimba la kombe la dunia na katika Kundi B, Nigeria iko katika nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kuishindilia Cameroon mabao 4-0 na kufikisha pointi 9

https://p.dw.com/p/2jL36
Africa Cup of Nations 2017 - Burkina Faso vs. Kamerun
Picha: picture-alliance/Anadolu Agency/O. Ebanga

Cameroon  mara  hii  itakuwa  mwenyeji  wa Nigeria  katika  mchezo  utakaofanyika  leo Jumatatu, wakati  kesho Algeria  itaumana  na  Zambia. Zambia  inashikilia  nafasi  ya  pili katika  kundi  hilo  la  B  ikiwa  na  pointi  4  baada  ya  kuiangusha Algeria  kwa  mabao 3-1. cameroon  ina  pointi  2  wakati  Algeria inashika  mkia  iliwa  na  pointi  1.

Cote d'Ivore  inashikilia  usukani  wa  kundi C ikiwa  na  pointi 7 ikifuatiwa  na  Morocco  yenye  pointi 5 , ambapo  kesho  Cote d'Ivoire inapambana  na  Gabon  na  Morocco  inamiadi  na  Mali . Wakati  huo  huo  Burkina  Faso  inayongoza  kundi  D kwa  pointi 5 itaumana  na  Senegal  ambayo  inashikilia  nafasi  ya  pili kwa  kuwa na  pointi  4 ikifuatiwa  na  Afrika  kusini  katika  nafasi  ya  tatu ikiwa  pia  na  pointi  4. Afrika  kusini  inapambana  na  Cape Verde kesho Jumanne.

Südafrika Fußball Nationalmannschaft
Timu ya taifa ya Afrika kusini "Bafana Bafana"Picha: P. Utomi Epkei/AFP/Getty Images

Uganda kidedea

Uganda  inaongoza  kundi E ikiwa  na  pointi 7 na  inafuatiwa  na Misri  yenye  pointi 6. Uganda  iko  mjini  Cairo  kupambana  kesho Jumanne  na  Misri , wakati  Congo Brazzaville  iliyoko  katika  nafasi ya  mwisho  ya  kundi  hilo  ina oneshana  kazi  na  Ghana  ambayo nayo  iko  nafasi  ya  tatu  ikiwa  na  pointi  2.

Shirikisho  la  kandanda  barani  Afrika  limesitisha  ziara  yake  ya ukaguzi  wake  wa  mwisho  nchini  Kenya  kutathmini  matayarisho kwa  ajili  ya  mashindano  ya  ubingwa  wa  kombe  la  mataifa  ya Afrika  kwa  wachezaji  wanaocheza  ligi  za  ndani  maarufu  kama CHAN, maafisa  wamesema  jana. 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / dpae / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman