1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Nigeria yafungua kiwanda kikubwa cha usafishaji mafuta

22 Mei 2023

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amefungua kiwanda kikubwa barani Afrika cha kusafisha mafuta yakiwepo matumaini kiwanda hicho kitasaidia nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa nishati kujitosheleza.

https://p.dw.com/p/4RfyA
Nigeria | LNG Anlage
Picha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Kiwanda hicho kimegharimu dola bilioni 19 kimejengwa na bilionea wa Afrika Aliko Dangote, katika mji ambao ni kituo cha kiuchumi, nchini humo wa Lagos. Kiwanda hicho kimeelezwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya usafishaji mafuta na kina uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku.

Baadhi ya wachambuzi wamesema kiwanda hicho kitaleta mabadiliko makubwa kwa sekta ya mafuta na gesi asilia nchini Nigeria, ambayo imekuwa ikijikokota kwa miaka mingi. Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanasema uwezo wa kiwanda hicho unaweza ukawa mdogo kutokana na wizi.

Soma pia: Nigeria yaifanyia mageuzi mikataba ya mafuta

Viwanda vingi vya usafishaji mafuta vinavyoendeshwa na serikali nchini humo havina matunzo mazuri na vinaendeshwa kwa viwango vya chini, hali inayoifanya nchi hiyo kuagiza mafuta yaliyosafishwa kutoka nje kwa matumizi yake.