1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaagiza kufunguliwa kwa mpaka wake na Niger

14 Machi 2024

Maafisa wa mpakani wa Nigeria wameamrishwa kuufungua tena mpaka wake na Niger uliofungwa tangu Agosti mwaka jana, kufuatia mapinduzi yaliyouleta uongozini utawala wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4dWt4
Niger
Nigeria yaagiza kufunguliwa kwa mpaka wake na NigerPicha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Waraka wa Idara ya Uhamiaji ya Nigeria umeonyesha kwamba maafisa hao wameamrishwa kuchukua hatua hiyo mara moja kutokana na uamuzi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu, hapo jana.

Mwezi uliopita ECOWAS iliamua kuuondoa vikwazo hivyo, ila mpaka huo ukawa bado umefungwa.

Niger, Mali, Burkina Faso zaunda kikosi cha pamoja kupambana na uasi

Vyanzo vya shirika la habari la Ufaransa AFP katika eneo hilo vimethibitisha kuwa mpaka huo katika jimbo la Katsina kaskazini mwa Nigeria bado ulikuwa umefungwa kufikia jioni ya jana.

Nigeria ilianza tena kusambaza umeme Niger mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi na kufikisha mwisho kukatika kwa umeme kulikokuwa kunashuhudiwa Niger tangu jeshi lilipochukua mamlaka.