Nigeria: Watu 15 wauwawa na Boko Haram
1 Novemba 2018Watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wamewauwa kiasi watu 15 katika shambulio dhidi ya vijiji kaskazini mashariki mwa Nigeria jioni ya Jumatano, wakaazi wa eneo hilo wameliambia shirika la habari la Reuters.
Vijiji hivyo viko nje kidogo ya mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na makao makuu ya juhudi za kupambana na kundi la Boko Haram pamoja na wapiganaji wengine wanaohusika na kundi hilo katika mataifa ya Afrika magharibi.
Mzozo huo umekuwapo katika eneo hilo kwa karibu miongo kadhaa. Licha ya taarifa hiyo ya serikali ya Nigeria tangu mwishoni mwa 2015 kwamba Boko Haram kwa kiasi kikubwa imeshindwa, wapiganaji hao bado wana uwezo wa kushambulia ndani na kuzunguka mji wa Maiduguri na sehemu nyingine kubwa za eneo hilo la kaskazini mashariki.