Nigeria: Watu 13 wamekufa kwa moto baada ya basi lao kuwaka
10 Agosti 2018Matangazo
Watu 13 wamekufa kwa moto baada ya basi walilokuwa wamepanda kuwaka moto baada ya kugongana uso kwa uso na trekta ya kuchimba mchanga na vifusi karibu na kituo cha mafuta kilichopo katika mji unaozalisha mafuta kwa wingi nchini Nigeria wa Port Harcourt.
Msemaji wa polisi wa jimbo la Rives Nnamdi Omoni ameliambia shirika la habari la AFP kwamba trekta hiyo iliteleza kutoka barabarani na kugongana uso kwa uso na basi hilo. Amesema, basi hilo lilikuwa linatoka Port Harcourt kuelekea Lagos likiwa na abiria 13 pamoja na dereva.
Ni mtu mmoja tu aliyepona kwenye ajali hiyo, huku miili ya abiria wengine ikiungua kabisa. Manusura wa ajali hiyo, ambaye hata hivyo alipata majeraha makubwa ya moto, alipelekwa hopitali kwa matibabu.