Nigeria ni kituo cha mwisho cha ziara ya Merkel barani Afrika
13 Julai 2011Wakati wa ziara ya pili katika bara la Afrika , kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia ataizuru Nigeria. Miezi mitatu tu baada ya kuchaguliwa Goodluck Jonathan kuwa rais wa nchi hiyo kansela ameonyesha ishara , kuwa Ujerumani inauona uchaguzi huu kama hatua muhimu kuelekea katika mfumo halisi wa kidemokrasia. Muhimu hata hivyo katika ziara hii ni suala la kiuchumi, ambapo Nigeria ikiwa na idadi kubwa ya wakaazi ni soko muhimu na katika nchi hiyo kunapatikana malighafi muhimu.
Nigeria ikiwa na idadi ya wakaazi milioni 150 ni yenye nguvu katika Afrika. Nchi hiyo inashindana na Angola katika nafasi ya kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta katika bara hilo. Na hata ikiwa kama msafirishaji mkubwa wa mafuta , Nigeria inazidi kuwa muhimu. Pamoja na hayo, Nigeria imeendelea kubakia muhimu pia katika uchumi wa dunia. Pato la mtu binafsi nchini Nigeria limefikia kiasi cha dola za Marekani 1,300 kwa mwaka. Nchini Afrika kusini ni mara sita ya kiwango hicho.
Mbali ya uchimbaji wa mafuta , lakini sekta hiyo imevurugika. Nigeria inapaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Na mchanganyiko baina ya ongezeko la uzalishaji mafuta na uagizaji unaifanya nchi hiyo kuwa kivutio kwa makampuni ya kigeni. Baada ya Marekani , umoja wa Ulaya ndio mshirika mkubwa wa pili wa kibiashara nchini Nigeria. Katika mji mkuu wa kibiashara Lagos , kuna ofisi ya masuala ya biashara za Ujerumani. Ofisi hii inaongozwa na Andre Rönne.
Muhimu kwa Ujerumani sio kuwa wa kwanza katika sekta ya mafuta na gesi, ambapo kila mmoja anafikiria kuhusu Nigeria, badala yake upande wa ujenzi, hususan miundo mbinu. Tunafaidika kwa kweli na uchimbaji wa mafuta, lakini nguvu za Ujerumani ziko mbali na sekta ya mafuta. Ambapo kwa kiasi kikubwa tunafaidika na kazi za usaidizi katika kandarasi.
Makampuni makubwa ya Ujerumani kama kampuni la ujenzi la Bilfinger-Berger pamoja na kampuni lake ndugu la Julius Berger , ama Siemens yako kote nchini Nigeria tangu muda mrefu uliopita. Pamoja na sekta ya ujenzi kuna sekta ya mawasiliano, huduma kwa jamii pamoja na uuzaji wa jumla , hizi ni sekta muhimu sana kwa Ujerumani. Mwaka jana biashara baina ya nchi hizi mbili ilifikia kiwango cha euro bilioni tatu. Kwa hiyo Nigeria ni nchi ya pili nyuma ya Afrika kusini katika ushirikiano wa kibiashara katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
kitu kinachowatisha wawekezaji ni hali mbaya ya rushwa nchini Nigeria. Katika viwango vilivyowekwa na shirika la Transparency International , Nigeria inashika mara kwa mara nafasi za nyuma kabisa. Andre Rönne anaiona hata hivyo kazi ya kigengo cha kupambana na rushwa kuwa ni muhimu.
Kitengo cha EFCC ni kitengo muhimu katika kupambana na rushwa na sio tu kupambana na rushwa katika uchumi, kwa upande wa Nigeria ama nje ya nchi, badala yake hata mapambano dhidi ya rushwa katika sekta ya kisiasa.
Pamoja na hayo idadi kubwa ya wanasiasa na pia wafanyakazi wa makampuni makubwa kutoka nje kama Siemens ama Bilfinger-Berger wamewajibishwa na kitengo kupambana na rushwa ama kufikishwa mahakamani kutokana na shutuma za ufisadi. Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Nigeria anayefanyia kazi zake nchini Saudi Arabia Musa Jega pamoja na hayo anaona ishara ndogo tu, kwa kupungua kwa rushwa nchini Nigeria.
Mwandishi : Thomas Mösch / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri : Mohammed Abdul Rahman