1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yaituhumu Ufaransa kutaka kuishambulia

10 Septemba 2023

Utawala wa kijeshi wa Niger umeituhumu Ufaransa kwa kukusanya wanajeshi na vifaa katika mataifa jirani ya Afrika ya magharibi kwa lengo la kuivamia kijeshi.

https://p.dw.com/p/4WA30
Niger Niamey | französische Luftwaffenbasis
Picha: ALAIN JOCARD/AFP/Getty Images

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa jana Jumamosi, msemaji wa utawala huo Kanali Amadou Abdramane amesema kuwa Ufaransa inaendelea kupeleka vikosi vyake katika nchi kadhaa za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Magharibi ECOWAS, kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya uchokozi dhidi ya Niger.

Soma pia: Sio wazi anayeiongoza Niger, baada ya wanajeshi waasi kumuondoa rais

Amefafanua kuwa Ufaransa imeshapeleka ndege za kijeshi, helikopta na vifaru 40 katika nchi za Ivory Coast na Benin na Senegal.

Uhusiano kati ya Niger na mkoloni wake wa zamani, Ufaransa uliingia dosari baada ya Paris kusimama upande wa Rais aliyepinduliwa mnamo mwezi Julai MohamedBazoum, na kusisitiza kutoutambua utawala wa kijeshi.