1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NIGER: watoto wakabiliwa na njaa

30 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEpl

Shirika la kutetea haki za watoto la umoja wa mataifa UNICEF limesema kuwa idadi kubwa ya watoto nchini Niger wana utapia mlo na kwamba wanakabiliwa na baa la njaa.

Tawi la UNICEF la Cologne limetoa ripoti kuwa takriban watoto 200,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wamekumbwa na utapia mlo.

Watu milioni 3.6 hawana chakula cha kutosha katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Ukame na nzige vimechangia pakubwa katika kutoweka kwa mavuno ya mwaka jana.

Shirika la Afya Duniani WHO limetoa ripoti kuwa visa vya ugonjwa wa kipindupindu vimeanza kutokea nchini Niger, watu watano wamefariki kati ya 49 walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo.