1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NIGER. Misaada ya chakula yaanza kuingia

24 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErR

Umoja wa mataifa umetoa ripoti kwamba misaada ya vyakula imeanza kuingia nchini Niger ambako watu zaidi ya milioni wanakabiliwa na baa la njaa.

Licha ya kutangaza hali ya hatari ya kukumbwa na njaa kutokana na ukame na uvamizi wa nzige mwaka uliopita wafadhili kutoka nchi za magharibi walipuuza ombi la Niger hadi siku za hivi karibuni.

Mkuu wa misaada ya kibinadamu wa umoja wa mataifa Jan Egeland amesema hali mbaya ya utapia mlo inayowakabili watoto imeishitua jamii ya kimataifa na kuwezesha kutolewa misaada kwa haraka.

Niger ni moja kati ya nchi masikini zaidi duniani na ukuzaji wake wa chakula nid uni kwani hautoshelezi raia wake.