Akiwa na miaka 37 tu, mwanasheria kijana Nicholaus Opiyo amekwishashughulikia kesi ngumu nchini Uganda. Akishirikiana na wenzake alifanikiwa kusimamia sheria ya mashoga nchini humo na kuwatetea wakosoaji wa serikali na wahanga wa mateso. Mwaka 2017, alipewa tuzo ya Germany-Africa kwa juhudi za kupigania haki za binadamu, katika kesi ambazo wengine hawakuwa tayari kuzishughulikia.