Niapoli, Italia. Polisi wasaka wauza madawa ya kulevywa.
21 Machi 2007Matangazo
Katika operesheni kubwa kabisa kuweza kufanyika dhidi ya makundi ya kihalifu , polisi wa Niapoli wamewakamata kiasi watu 200 jana Jumanne, ikiwa ni pamoja na katika baadhi ya sehemu familia nzima.
Maafisa wamesema kuwa lengo lilikuwa kuvunja biashara inayozidi kupanuka kusini mwa Italia ya madawa ya kulevywa, inayoendeshwa na kundi ya kihalifu la Mafia, wanaojulikana kama Camorra.