1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NIAMEY:Serikali ya Niger yavunjwa

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBw2

Serikali ya Niger imevunjwa baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani nayo.Hatua hiyo ilisababishwa na kesi ya rushwa katika wizara ya elimu.Mawaziri wawili wa zamani walidaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa jambo lililopelekea kujiuzulu kwa Baraza la mawaziri huku Waziri mkuu Hama Amadou kutarajiwa kujiuzulu hii leo.

Rais Mamadou Tanja analazimika kutafuta mrithi wake au kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi katika kipindi cha siku 45.Kesi hiyo ya udanganyifu wa rushwa ya mwaka 2005 ilihusisha euro milioni 1.7 kwa mujibu wa Waziri wa Sheria Maty Elhadj Moussa aliyesema hayo mwaka jana.