Niamey. Shehena ya kwanza ya chakula cha msaada yawasili nchini Niger.
22 Julai 2005Matangazo
Shehena ya kwanza ya msaada wa chakula imewasili nchini Niger, ambako watu milioni 3.5 wanakabiliwa na njaa na ukame.
Ndege ya kijeshi ya Ufaransa imetua katika mji wa kati kusini mwa nchi hiyo wa Maradi ikiwa imebeba tani kadha za chakula.
Jan egeland, kiongozi wa kitengo cha uratibu wa masuala ya kibinadamu ya umoja wa mataifa , ameishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka dhidi ya tatizo hilo, ambalo linatishia maisha ya watoto 150,000.
Shirika la kutoa misaada la Oxfam limesema kuwa watu wanawalisha watoto wao majani na ukoka. Mavuno yanatarajiwa katika muda wa miezi mitatu ijayo.