1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niamey. Rais wa Niger kuzuru maeneo yaliyoathirika na njaa.

26 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqk

Rais wa Niger Tandja Mamadou akikabiliwa na shutuma nchini mwake kwa kushindwa kuelezea tatizo la njaa linalowakabili mamilioni ya watu, anapanga kuzuru baadhi ya maeneo ambayo yameathirika zaidi wiki hii.

Makundi ya kijamii yamemshutumu rais Mamadou kwa kushindwa kuieleza hali hiyo ya ukosefu wa chakula inayowakabili watu milioni 3.5 nchini Niger kwa kuhofia kuidhalilisha serikali yake, licha ya kuwa wale wanaomuunga mkono wanasema amefanya vya kutosha kuitangaza hali hiyo.

Mamadou ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi ambaye alichaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi wa Desemba , atatembelea majimbo ya kaskazini ya Tahoua leo Jumanne na Agadez siku ya Jumatano kuangalia hali ya matatizo hayo nchini Niger, nchi kame iliyoko katika pembe ya kusini ya jangwa la Sahara.