NIAMEY: Misaada inaanza kuwasili Niger
25 Julai 2005Matangazo
Chakula na misaada mingine ya kiutu imeanza kufika nchini Niger ambako mamilioni ya watu wanakabiliwa na kitisho cha njaa.Maombi ya misaada yalidharauliwa na wafadhili wengi wa magharibi mpaka hivi karibuni.Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia misaada ya kiutu,Jan Egeland amesema,ahadi za misaada ziliongezeka sana wiki iliyopita.Akasema kuwa jumuiya ya kimataifa haikuamaka mpaka ilipoanza kuona picha za watoto wanaokufa.Niger,nchi iliyo masikini kabisa duniani,mwaka jana ilikabiliwa na balaa la nzige na ukame pia.