Ni muhimu kutuma kikosi Somalia
20 Novemba 2007
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana limesema ni muhimu kuendelea kupanga uwezekano wa kutuma kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Somali licha ya maoni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa huo kwamba kikosi hicho kwa sasa sio kitu kinachoweza kuzingatiwa.
Ban Ki-moon amesema mapema mwezi huu kwamba hali ya usalama ni mbaya kwamba ilikuwa haiwezekani hata kutuma timu ya kiufundi kutathmini hali ya Somalia ambayo ni hatua muhimu katika kuandaa mipango ya kutuma wanajeshi wa kulinda amani.
Rais wa Baraza la Usalama balozi wa Indonesia kwa Umoja wa Mataifa Marty Matalegawa amesema baraza hilo pia linatambuwa haja ya kutowa msaada mubwa wa kifedha,vifaa na kiufundi kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika ambacho hadi sasa kimetuma wanajeshi 1,600 tu kati ya wanajeshi 8,000 waliopangwa kutumwa nchini Somalia.