1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neymar aurefusha mkataba wake na Barca

1 Julai 2016

Kwingineko viwanjani, kipindi cha ununuzi wa wachezaji barani Ulaya limeanza rasmi. Mchezaji nyota wa Barcelona Neymar amesaini mkataba mpya utakaomfikisha mwaka wa 2021

https://p.dw.com/p/1JHZw
England Fußball UEFA Champions League FC Arsenal - FC Barcelona
Picha: Getty Images/S. Botterill

Ni wakati ambapo tunatarajia kuona vilabu mbalimbali hasa vya ligi ya kuu ya kandanda England, Uhispania na Ujerumani vikitumia kiasi kikubwa cha fedha katika biashara ya wachezaji wapya.

Barcelona imeurefusha mkataba wa mshambuliaji Neymar hadi mwaka wa 2021. Neymar mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Barca mwaka wa 2013 kutoka klabu ya Santos ya Brazil. Ameifungia timu hiyo mabao 55 katika mechi 93.

Manchester City ilifanya usajili wake wa pili chini ya kocha Pep Guardiola, kwa kuinasa saini ya Mhispania Nolito kutoka klabu ya Celta Vigo. Tayari Pep alimsajili kiungo Mjerumani Ilkay Gundogan.

Wapinzani wao Manchester United wamemsaini aliyekuwa mshambuliaji wa Paris-Saint Germain Zlatan Ibrahimovic. Aidha kiungo wa Dortmund Herikh Mkhitaryan anaelekea Old Trafford.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef