1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEWYORK:Shirika la WHO lahitaji fedha zaidi kupambana na Ukimwi duniani

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEz1

Shirika la Afya duniani WHO limekiri kwamba huenda likashindwa kufikia lengo lake la kuwapatia waathiriwa kiasi cha milioni tatu wa Ukimwi, dawa za kupunguza makali Ugonjwa huo ifikiapo mwisho wa mwaka 2005.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limearifu kwenye ripoti yake kwamba ni watu kiasi ya milioni moja tu wanaopata dawa hizo katika mataifa yanayoendelea.

Kiasi cha dolla bilioni 27 zimetolewa kupambana na Ukimwi duniani katika mwaka 2005 hadi 2007 lakini kwa mujibu wa shirika hilo kiasi cha dolla bilioni 18 zaidi zinahitajika hivi sasa kufanikisha lengo hilo.

Watu milioni 40 wameambukizwa viini vya maradhi ya Ukimwi duniani kote.