1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New_york: Nchi 18 za Afrika,Asia na latin Amerika zinalaumiwa na ...

16 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFio
wanaharakati wa haki za binadam kuendelea kuwatumia watoto vitani.Idadi ya watoto wanaotumiwa vitani imeongezeka mwaka jana nchini Ivory Coast,Liberia na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo-imetajwa ndani ya ripoti ya shirika la kukomesha watoto wasitumiwe vitani-shirika lililoundwa na Amnesty International pamoja na Human Rights Watch.Kabla ya hapo,muakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan,bwana Olara Otunnu alilitolea mwito baraza la usalama lipitishe hatua kali dhidi kutumiwa watoto vitani.Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepanga kulijadili suala hilo jumanne ijayo mjini New-York.