NEW YORK:Warranti yatolewa ya kukamatwa viongozi 5 wa LRA
7 Oktoba 2005Mahakama ya kimataifa mjini The Hague kwa mara ya kwanza imetoa warranti ya ukamataji.
Kwa mujibu wa William Lacy Swing,mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Warranti hiyo imetolewa kwa viongozi watano wa Kundi la jeshi la waasi wa Uganda LRA.
Amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba warranti hizo zilipelekwa nchini Kongo,Uganda na Sudan mnamo wiki iliyopita.
Hata hivyo Swing amesema hawezi kutoa majina ya viongozi hao watano wanaotakiwa kukamatwa lakini waangalizi wanasema kuna uwezekano mmoja kati ya watano hao akawa ni kiongozi wa LRA Joseph Kony.
Waasi wa LRA wamekuwa wakishutumiwa kwa kuendeleza maouvu dhidi ya raia tangu mzozo wao na serikali ya Uganda kuanza takriban miaka 20 iliyopita.