NEW YORK:Wanajeshi wa Ethiopia wadaiwa kuwanyanyasa raia wa Gambella
24 Machi 2005Matangazo
Kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini New York,limesema wanajeshi wakiethiopia wamewanajisi na kuwatesa mamia ya watu kusini mashariki mwa nchi hiyo katika eneo la Gambela tangu mwezi Desemba mwaka 2003.
Ripoti ya kundi hilo ya kurasa 64 iliyotolewa leo, uchunguzi huo uliofanywa mwezi Desemba iliyopita unaonyesha kuwa vitendo dhidi ya jamii ya waanuak huenda ikazidisha uhalifu dhidi ya binadamu.
Hata hivyo maafisa wa serikali ya Ethiopia hawakupatikana mara moja kutoa msimamo wao kuhusu ripoti hiyo lakini awali waziri mkuu Meles Zenawi alipinga madai ya ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali wanajeshi sita wanatazamiwa kushtakiwa kwa kuhusika katika mzozo wa Gambella.