1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Syria na Lebanon zimehusishwa na mauaji ya Hariri

21 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEPm

Ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa inasema kuwa maafisa wa usalama wa ngazi ya juu wa Syria na Lebanon,kwa uhakika fulani walihusika na mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafik Hariri.Kwa mujibu wa ripoti ya mwendesha mashtaka Detlev Mehlis,mauaji ya Hariri hapo tarehe 14 Februari yalikuwa na utata na ni vigumu kuamini kuwa idara za upelelezi za Syria na Lebanon hazikuwa na habari yo yote.Ripoti hiyo ya kurasa 53 imesema uchunguzi bado haujakamilika na lazima uendelee kufanywa na wakuu wa kisheria na usalama wa Lebanon.Siku ya Alkhamisi nchini Lebanon,kiasi ya wanajeshi na askari 10,000 waliwekwa katika hali ya tahadhari kwa kile kilichoitwa “hali ya hatari isiyo rasmi”.