NEW YORK.Muda wa kikosi cha kulinda amani mpakani mwa Eritrea na Ethiopia waongezwa
30 Septemba 2006Matangazo
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepitisha bila ya kupingwa hatua ya kuongeza muda hadi miezi minne kwa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani katika mpaka wa Eritrea na Ethiopia huku umoja huo ukitafakari mabadiliko katika mamlaka ya kikosi hicho katika eneo hilo.