1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.Mazungumzo juu ya Sahara Magharibi yamalizika bila mafanikio

20 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqB

Wajumbe wa Morocco na wa chama cha ukombozi , wa Sahara Magharibi , Polisario wamemaliza mazungumzo yao mjini New York lakini bila ya kufikia mapatano.

Hatahivyo wajumbe hao wamekubaliana kukutana tena mwezi wa agosti ili kutatua mzozo wao wa Sahara Magharibi.

Sehemu hiyo ilichukuliwa kwa nguvu na Morocco, baada ya Uhispania iliyokuwa mkoloni kuondoka.

Morocco imependekeza kufanyika kura ya maoni juu ya kuipa Sahara Magharibi madaraka ya kujisimamia lakini chini ya udhibiti wa Morocco.

Chama cha Polisario kinapinga mpango huo na badala yake kinataka watu wa Sahara Magharibi wapewe haki ya kujitawala.