New-York:Eritrea na Ethiopia zalaumiwa na baraza la usalama
15 Machi 2005Baraza la usalama la umoja wa mataifa limerefusha kwa miezi sita,hadi september 15 ijayo,shughuli za tume ya kusimamia amani UNMEE kati ya Ethiopia na Eritrea.Baraza la Usalama la umoja wa mataifa liemzitaka nchi hizo mbili za pembe ya Afrika ziache kukusaanya wanajeshi karibu na mpaka wao wa pamoja na waache mitindo ya kutishana.Kwa mujibu wa ripoti ya tume ya Umoja wa mataifa ya UNMEE,Ethiopia imezidisha idadi ya wanajeshi wake mpakani tangu january iliyopita.Wanajeshi 4000 wa umoja wa mataifa wanalinda eneo la mpakani linalozitenganisha ethiopia na eritrea.Watu wasiopungua 70 elfu wameuwawa kufuatia vita vya miaka miwili vilivyoripuka mwaka 1998.Nchi zote mbili zimetia saini makubaliano ya Algiers mwaka 2000 kuhusu mipaka mipya kati yao,mipaka iliyochorwa na kamisheni ya kimataifa mwaka 2002 lakini hadi sasa hakuna anaeifuata.