1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Dola milioni 30 zaombwa katika Umoja wa Mataifa,kuwasaidia waliovunjiwa makazi yao Zimbabwe.

28 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWr

Umoja wa Mataifa umeomba karibu dola milioni 30 zitakazotumika kwa mahitaji ya msaada wa kibinadamu kwa watu waliovunjiwa makazi yao nchini Zimbabwe.

Maombi hayo yalitakiwa awali tangu mwezi wa August,lakini Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe awali alikataa fedha hizo kuingia nchini mwake,baada ya kuishutumu ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa tarehe 2 mwezi wa Julai,iliyokuwa ikiitupia lawama serikali ya Zimbabwe kwa kuyavunja makazi hayo,ambapo ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliita ni vitendo vya ukatili na visivyoendana na haki za binadamu,ambapo watu 700,000 waliathirika na bomoa bomoa hiyo.

Maombi hayo mapya ya fedha yalipelekwa mbele ya Umoja wa Mataifa na balozi Jan Egeland,mratibu wa matukio ya dharura wa Umoja wa Mataifa na fedha hizo zinakusudia kuwanufaisha watu 300,000.

Rais Robert Mugabe amemwalika Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan kutembelea Zimbabwe na Bwana Annan anafikiria mwaliko huo,huku kukiwa na mgawanyiko miongoni mwa maafisa wa Umoja wa Mataifa,iwapo Bwana Annan aende au akatae mwaliko huo.

Bwana Egeland anatazamiwa kuitembelea Zimbabwe kabla ya kumalizika mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.