NEW YORK: Wito wa kuwa na uchaguzi huru Lebanon
28 Septemba 2007Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa mwito kwa Lebanon kufanya uchaguzi wa rais tarehe 23 Oktoba kama ilivyopangwa.Taarifa iliyotolewa na wanachama 15 wa baraza hilo imesema,uchaguzi uwe huru na wa haki.Ufanywe bila ya machafuko na vile vile nchi za nje zisiingilie kati.
Kuna hofu kuwa mvutano kuhusu mgombea urais, huenda ukasababisha kuundwa kwa serikali mbili hasimu.Wagombea uchaguzi wanahitaji kupata wingi wa theluthi mbili katika bunge la wajumbe 127,ili kuweza kuchaguliwa kwa duru ya kwanza ya uchaguzi huo.Awamu ya rais wa hivi sasa,Emile Lahoud anaelewana na Syria,inamalizika mwezi wa Novemba.