NEW YORK Walinda amani zaidi kupelekwa Haiti
23 Juni 2005Matangazo
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepitisha uamuzi wa kuwapeleka walinda amani 1,000 zaidi nchini Haiti, huku uchaguzi wa mwezi Oktoba ukikaribia nchini humo.
Uamuzi huo umefuatia hatua ya waziri mkuu wa serikali ya mpito Gerard Latortue kufanya mabadiliko serikalini ili kujenga imani na raia huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuwa mbaya. Mamlaka ya jeshi hilo ilirefushwa hadi mwezi Februari mwaka ujao wakati rais mpya wa Haiti anapotarajiwa kuchukua madaraka.
Walinda amani wa umoja wa mataifa walipelekwa nchini Haiti baada ya rais wa zamani Jean Bertrand Aristide kuihama nchi hiyo.