1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Waislamu wa siasa kali Somali watengwe

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrZ

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka nchi zote kuacha kuunga mkono Waislamu wa siasa kali nchini Somalia na kutowa wito wa kuitishwa na mapema kwa mkutano wa usuluhishi wa kitaifa uliochelewa kuitishwa kwa muda mrefu ili kuanza kuponya majeraha ya mzozo uliodumu kwa miaka 16 nchini humo.

Baraza hilo pia limesisitiza haja ya dharura kwa Umoja wa Mataifa kuanza kupanga uwezekano wa kuweka jeshi la kulinda amani nchini Somalia kuchukuwa nafasi ya kikosi cha Umoja wa Afrika ambacho hivi sasa kina wanajeshi 1,500 wa Uganda nchini Somalia.

Wakati huo huo shambulio la bomu la mkono limeuwa watu wanne na kujeruhi wengine sita wakati wakiangalia video katika mji wa magharibi wa Baidoa.

Bomu hilo limerushwa wakati wa usiku kwenye onyesho la video la mchezo kihindi.

Wanamgambo wa Kiislam ambao wamekuwa wakipambana na serikali ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika wanapinga sinema za kihindi na za mataifa ya magharibi kwa hoja kwamba zinapotosha maadili katika nchi hiyo ya Kiislam yenye watu milioni 10.