NEW YORK: Vikosi vya Syria vimeshaondoka Lebanon
24 Mei 2005Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amesema,Umoja huo umethibitisha kuwa Syria imeshaviondosha vikosi vyake vyote kutoka nchi ya jirani Lebanon.Syria ilivihamisha vikosi vyake kuambatana na Azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi wa Septemba.Azimio hilo lililopendekezwa na Ufaransa na Marekani lilitoa muito kwa Syria kuondosha vikosi vyake vyote kutoka Lebanon.Damascus iliamua kuvihamisha vikosi vyake baada ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafiq Hariri kuauwa tarehe 14 mwezi wa Februari.Damascus na serikali ya zamani ya Lebanon iliyokuwa ikiungwa mkono na Syria zililaumiwa na wengi kwa mauaji hayo.