New York. Umoja wa mataifa watuma timu nyingine ya watu kuchunguza iwapo Syria imepeleka majasusi wengine Lebanon.
11 Juni 2005Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan ameamua kutuma kundi la uchunguzi la umoja huo kwenda tena Lebanon kuangalia iwapo majasusi wa Syria bado wako nchini Lebanon.
Hii inakuja baada ya ikulu ya Marekani kusema kuwa inazotaarifa kuwa Syria imetayarisha orodha ya wanasiasa wa Lebanon ambao watauwawa.
Maafisa wa Syria wamekanusha madai hayo.
Kundi la wataalamu wa umoja wa mataifa limeripoti mwishoni mwa mwezi wa May kuwa Syria imeondoa kabisa majeshi yake baada ya kuwako nchini Lebanon kwa muda wa miaka 29.
Lebanon hivi sasa inafanya uchaguzi wa jimbo baada ya jimbo ambao utamalizika hapo Juni 29, uchaguzi wa kwanza katika muda wa miongo mitatu bila ya kuwapo majeshi ya Syria nchini humo.