NEW YORK: Umoja wa mataifa walaani mauaji ya waziri wa viwanda wa Lebanon,Pierre Gemayel
22 Novemba 2006Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani kwa kauli moja mauaji ya waziri wa viwanda wa Lebanon, Pierre Gemayel na kuzitolea mwito pande zote nchini Lebanon na katika eneo zima kuonyesha ustahamilivu.
Katika taarifa iliotayarishwa na Ufaransa na ambayo imesomwa na balozi wa Peru kwenye Umoja wa mataifa, Jorge Voto-Bernales, wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamesema mwanasiasa huyo mashuhuri, mkristu, alikuwa mtetezi wa uhuru na . balozi wa Marekani kwenye Umoja wa mataifa John Bolton, ameongeza kusema wauaji wake wapaswa kukamatwa. Mauaji ya Pierre Gemayel, yametokea wakati baraza la usalama la Umoja wa mataifa limepitisha pendekezo la kuundwa mahakama ya kimataifa kuwasikiliza washukiwa wa mauaji ya aliekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Rafic Hariri, alieuawa mwezi Februari mwaka 2005.