NEW YORK: Umoja wa mataifa wailaumu Eritrea kuingia katika eneo la usalama kati yake na Ethiopia
17 Oktoba 2006Matangazo
Umoja wa mataifa umeituhumu nchi ya Eritrea kuwapeleka wanajeshi na vifaru vya kijeshi katika eneo la usalama lililowekwa kati ya nchi hiyo na Ethiopia. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, ameitaka Eritrea iwaondowe wanajeshi wake kutoka eneo hilo la usalama ili kuepuka kuhatarisha mkataba wa kukomesha mapigano uliofikiwa miaka 6 iliopita. Wanajeshi wa Umoja wa mataifa wanashika doria kulichunguza eneo la kilomita 1000 lililotengwa na Umoja wa mataifa kati ya nchi hizo mbili katika juhudi za kuvimaliza vita vya miaka miwili ambavyo vilisababisha mauaji ya watu zaidi ya 70,000.