1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Ripoti juu ya Zimbabwe yajadiliwa

28 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqD

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejadili ripoti juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali ya Zimbabwe za kuwavunjia wananchi makaazi yao .

Ripoti hiyo iliyowasilishwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa bibi Anna Tibaijuka wa Tanzania imejadiliwa licha ya upinzani wa nchi za kadhaa.

Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti hiyo kwamba maalfu ya watu sasa hawana pa kukaa baada ya nyumba zao kuvunjwa na kwamba hatua hiyo imesababisha madhila makubwa kwa watu hao.

Marekani na Uingereza ziliongoza kampeni ya kuwezesha kujadiliwa kwa taarifa hiyo lakini nchi kadhaa ikiwa pamoja na Urusi na China zilipinga.

Wajumbe wa nchi hizo wamesema kuijadili ripoti hiyo ni kujiingiza katika mambo ya ndani ya Zimbabwe.

Tanzania pia ilipinga kujadiliwa kwa

ripoti hiyo.

.